Prof. Ibrahim Lipumba |
Prof. Lipumba akipata maelekezo katika banda la NEEC sabasaba |
Prof. Lipumba akipata maelekezo katika banda la NEEC sabasaba |
Dr. Joyce Chonjo, Mkurugenzi NEEC |
Serikali na taasisi binafsi zimemetakiwa kuacha kuagiza
samani za maofisini nje ya nchi na badala yake wanunue samani za kitanzania
zinazotengenezwa hapa nchini ili kukuza soko la ndani na kuongeza ajira kwa
vijana
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa chama cha wanachi CUF
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye pia ni mtaalam wa maswala ya uchumi wakati
akitembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara jijini Dar es salaam
Profesa Lipumba amesema ni wakati muafaka wa kuacha
kung’ang’ana na bidhaa za nje ya nchi kwa kuwaunga mkono vijana kwa kutumia bidhaa za ndani ambazo zinaubora
wa hali ya juu. pia amesema maonyesho kama haya yana umuhimu mkubwa katika
kutangaza bidhaa za ndani na kukuza uchumi wa nchi unaoenda sambamba na kukua
kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja
Nae Dr. Joyce Chonjo ambaye ni mkurugenzi wa baraza la taifa la
uwezeshaji amesema zaidi ya wajasiriamali 38 katika maonyesho hayo wamenufaika
na mfuko wa uwezeshaji ambapo zaidi ya mikoa 5 inatarajiwa kunufaika na bajeti
ya mwaka huu.
Amesema pesa hizo pia zitatumika katika kutoa mokopo,
mafunzo, katika kufanya utafiti na uhamasishaji kwa kuwa kila siku uwezeshaji
wa vikundi na mtu mmoja mmoja unasomga mbele
No comments:
Post a Comment