Mh. Bernard Membe |
SERIKALI imesema inafanya uchunguzi kubaini kama meli 11 za Iran zinazotumia bendera ya Tanzania na kusafirishia mafuta kutoka nchini humo zina uhalali wa kufanya hivyo.
Meli za kampuni ya Irani ya NITC zinatumia bendera ya Tanzania na kwa taarifa za awali ni kwamba meli hizo zimesajiliwa Zanzibar kama kampuni ya nchini Uingereza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe amesema uchunguzi huo umeshirikisha serikali ya Muungano, Serikali ya Zanzibar na nchi nyingine wanachama wa umoja wa mataifa.
Waziri Membe anasema kuwa endapo meli hizo zitabainika kuwa zilisajiliwa Tanzania zitafutiwa vibali vyote mara moja.
Waziri Membe ameongeza kuwa uamuzi huo hautokani na shinikizo la barua ya June 29, mwaka huu ya Mbunge wa Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje Howard Berman.
No comments:
Post a Comment