Aloyce Masanja – Mkurugenzi - RUBADA |
Francisco Luz – Barozi wa Brazil |
Mamlaka ya uendeshaji wa bonde la mto Rufiji RUBADA umesaini
mkataba wa makubaliano ya awali ya kuzalisha nishati ya umeme kupitia mradi wa
stiegler’s Gorge na kampuni ya Odebretch Group ya Brazil
Mkataba wa makubaliano ya mradi huo umesainiwa jijini Dar es
salaam na mkurugenzi wa RUBADA Aloyce Masanja na mkurugenzi wa biashara wa
Odebretch Fernando Soares.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo mkurugenzi wa RUBADA Aloyce Masanja amesema
mradi huo uko katika hatua muhimu na
ukikamilika utaleta manufaa makubwa ya kibiashara na kiuchumi kwa taifa
Francisco Luiz ni Balozi wa Brazil hapa nchini amesema mradi
huo ni chachu katika kuchochea kasi ya maendeleo ya nishati hapa nchini kwa
kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo na kupunguzia adha ya kukosekana kwa umeme.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya uendeshaji
wa bonde hilo Profesa Raphael Mwalyosi amesema wanategemea serikali itasimamia
na kuhakikisha mradi huo wa stiegler’s Gorge unakamilika kwa wakati
Makubaliano hayo yanatoa fursa ya kuanza kufanyika kwa
upembuzi yakinifu kupitia ule uliofanywa awali na Norway mwaka 1980 na
kufanyika maboresho ambapo baada ya miezi 6 kampuni hiyo itatoa ripoti ya
kwanza itakayoonyesha mda wa kuanza na kumalizika kwa mradi huo.
No comments:
Post a Comment