Tuesday, August 28, 2012

INDIA KULETA WATAALAM WA AFYA KUTOA HUDUMA KWA BEI NAFUU

Na Joyce Mwakalinga

Ubalozi wa India nchini Tanzania unatarajia kuleta wataalamu wa afya Tanzania kutoka hospitali kubwa nchini India watakaotoa huduma za afya kwa bei nafuu.

Ugeni huo ulioandaliwa na taasisi ya shirikisho la biashara na maonyesho la nchini India IMTD utawasili jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi huu.


Wataalamu hao wa afya kupitia shirika hilo la nchini india la Indian Medical Tourism Destination IMTD watatoa huduma hizo kupitia maonyesho yatakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa ubalozi wa india Nchini Tanzania Debnath Shaw anasema hatua ya utoaji wa huduma hizo zitawasaidia watanzania wengi ambao wamekuwa wakifuata matibabu nchini mwao.

Naye mkurugenzi wa shirikisho la wafanyabiashara wa viwanda nchini India FICCI Vivek Kodikal anaelezea ni jinsi gani watanzania wanatumia gharama kubwa kwa kutibiwa India.

Maonyesho hayo yatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa siku mbili mfululizo za Agost 30 na 31.

Watakaoshiriki ni pamoja na wataalamu mbalimbali wa afya kutoka nchini Tanzania, wadau katika sekta ya afya kutoka nchini india ambao ni pamoja na wawakilishi kutoka hospitali na vituo vikubwa vya afya.

No comments:

Post a Comment