Charles Singili Mkurugenzi Mtendaji Azania Bank |
Benki ya Azania ya hapa nchini imezindua huduma mpya za
kibenki kwa kutumia internet (Internet Banking) kwa lengo la kuwawezesha wateja
wake kupata huduma za fedha kwa uraisi.
Kuzinduliwa kwa huduma hizo kutasaidia upatikanaji wa
taarifa muhimu za akaunti za wateja wa benki hiyo na hivyo kuwawezesha kupata
huduma kwa haraka.
Kwenye makao makuu wa Benki ya Azania Jijini Dar es salaam,
mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo alizindua huduma hii mpya na hivyo kutoa fursa kwa wateja wa benki
hiyo kupata taarifa za akaunti zao popote walipo.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano
Tanzania profesa John Nkoma amewataka wateja wanaotumia huduma za mitandao ya
internet kuwa makini na kutunza namba zao za siri ili kuepusha wizi wa kutumia
mtandao.
Huduma hiyo itamuweza mteja mwenye akaunti kulipia huduma
mbalimbali kama Luku, kulipia huduma ya Maji kwa Dar es salaam – DAWASCO, DSTV
na hata kununua muda wa maongezi kwenye siku yake bila kwenda kwenye tawi la
Benki.
Benki hiyo ambayo pia inamilikiwa serikali inaendelea na
maboresho ya huduma zake ili kuwawezesha wateja wake kutumia huduma hizo bila
usumbufu wowote.
No comments:
Post a Comment