Umoja wa Ulaya na serikali ya Tanzania zimetiliana saini ya makubalino ya msaada wa shilingi bilioni 250 kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya barabara, maji safi pamoja na kuimarisha demokrasia ili kuinua uchumi wa Tanzania.
Katika makubaliano hayo yaliyofanyika ikulu jijini dar es salaam
jumla ya mikataba sita ilisainiwa na waziri wa fedha William Mgimwa pamoja na
kamishna wa maendeleo ya Umoja wa Ulaya kwa niaba ya marais wa Tanzania pamoja
na umoja huo.
Mkataba wa kwanza ambao ni euro million45 unakwanda katika sekta
ya usafirishaji, euro million22 katika kuimarisha barabara za vijijini na
euro milioni 3 zinakwenda katika kuimarisha demokrasia visiwani Zanzibar
Nyingine ni euro milioni 2.5 zimetengwa katika kuimarisha
ushirikiano na sera za umoja huo nchini Tanzania pamoja na euro milioni
51.51 ambazo zitatumika kwa lengo la kutimiza malengo ya milenia mdg kwa kupata
maji safi katika mikoa ya lindi, rukwa na kigoma.
Akiongea mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo rais wa
kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barroso amesema kuwa mikataba hiyo ipo wazi na
inalenga kusaidia maeneo ambayo yameonekana kukwamisha maendeleo kwa kiasi
kikubwa.
Naye rais Jakaya Kikwete amesema kuwa miradi hiyo inalenga
kumaliza matatizo ya maji hasa katika mikoa iliyotajwa ambapo bado wananchii
wake wameonekana kukwazwa na matatizo hayo.
Tangu kujiunga na kamisheni ya umoja wa ulaya mwaka 1975
tanzania imeweza kupata msaada wa euro billion1.8 sawa na shilingi trillion 3.8
ambazo zimepelekwa katika mahitaji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment