Friday, July 20, 2012

ADA YA ZIMAMOTO SASA KUKATWA KWENYE ROAD LICENSE

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA  kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji  nchini limefanikiwa kwa kiasi kikubwa zoezi la kukusanya ada ya ukaguzi wa magari na vyombo vingine vinavyoingia nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA Allan Kiula amesema mapato ya ukaguzi yatalipwa kwa TRA na mteja atapatiwa stika inayojumuisha malipo yote

Amesema Mfumo huo ulianza rasmi june tano mwaka huu ambapo maafisa wa zimamoto walikuwa wakikusanya mapato hayo katika ofisi za TRA na kufanikiwa kuongeza mapato kwa kiasi kikubwa lakini kumekuwa na usumbufu kwa pande zote mbili

Kaimu mkurugenzi huyo amesema kwa sasa mitambo ya TRA imeongezewa kipengele cha zimamoto hivyo kuanzia julai 23 mwaka huu watakaolipia leseni ya matumizi ya barabara watakatwa moja kwa moja ada ya zimamoto kitendo kitakachopunguza usumbufu kwa wananchi

Akizungumzia mapato ya mwaka 2011/2012 mhasibu wa jeshi la zimamoto amesema walikadiriwa kukusanya bilioni 2.5 na walikusanya bilioni 1.6 na kwa maboresho ya sasa wanategemea kufikia makadirio ya mwaka huu kama anavyobainisha

Amesema kuanzia miaka ya tisini na mwaka 2004 walinunua magari yanayoweza kubeba lita elfu 8 na ya lita elfu 16 na kubainisha mikakati ya kujenga vituo vya zimamoto katika meneo ya Tabata, Mbezi Luis, Tegeta, Mbagala, Kigamboni, Gongo la Mboto, na Mwenge kutoka katika asilimia 70 ya mapato yatakayokusanywa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment