Friday, July 20, 2012

LIPUMBA AITAKA SERIKALI KUANGALIA UPYA UTENDAJI WA SUMATRA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba ameitaka serikali kuhakikisha inaangalia upya utendaji wa mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini Sumatra kutokana na kushindwa kuwajibika katika majanga  mbalimbali.

Prf Lipumba ameyasema hayo jijini dar es salaa wakati akiongea na waandishi wa habari juu ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit. jumatano ya wiki hii.

Profesa Lipumba amesema kuwa nchi ina mapungufu makubwa katika kitengo cha taifa cha uokoaji kutokana na kutokuwa na zana za kisasa za uokoaji kiasi cha kutegemea msaada kutoka nchi ya afrika kusini pindi ambapo kunatokea ajali na hivyo kusababisha kushindwa kuokoa abiria.

amesema kuwa kuna umuhimu wa serikali kuangalia utendaji wa Sumatra lakini pia kuhakikisha kunakuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya kituo cha hali ya hewa na chombo cha kusimamia usafirishaji ili kuepuka vifo kwa wananchi kama utendaji wa  mamalka ya hali ya hewa unavyofanyika.

Ameongeza kuwa licha ya tume ya maafa kufika mapema lakini ilishindwa kutoa msaada wa kutosha kutokana na kutokuwa na zana za kisasa za uokoaji pamoja na wataalam waliobobea katika  majanga ya aina hiyo.

Meli hiyo ambayo ilkuwa ikitokea bandari ya dar es salaam kuelekea Zanzibar ikiwa na abiria 290 wakiwemo watoto wadogo wapatao40 ilizama katika kisiwa cha chumbe kutokana na dhoruba kali na kupelekea ilale kwa ubavu kwa muda mfupi na baadaye kugeuka juu kuelekea chini kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.

Meli ya Mv Skagit ilitengezwa mwaka1989 na kufanya kazi seattle Washington marekani na mwaka 2006 iliachishwa kufanya kazi lakini baadaye ikauzwa Tanzania ambapo ilisajiliwa Zanzibar na baadaye ilikwenda kufanyiwa marekebisho Mombasa kwa ajili ya kuiongezea urefu kitendo kilichafanya meli hiyo kuyumba pindi inapopakia abiria.

No comments:

Post a Comment