SERIKALI
imekiri kuwepo kwa mapungufu katika Wizara mbili ikiwepo Wizara ya ardhi na
maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya maliasili na utalii hali inayosababisha
utata na migogoro miongoni mwa jamii inayozunguka misitu ya Pugu na Kazimzumbwi
Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Sehemu ya Msitu wa Pugu |
Migogoro
ya mipaka inaendelea kwa wakazi wanaoizunguka misitu hiyo na kusababisha
kuvunjika kwa amani kutokana na baadhi ya wakazi kuvamia msitu wa kazimzumbwi
na kuchoma moto maeneo ya msitu huo kwa madai kuwa Wizara ya maliasili na
utalii inawaondoa katika maeneo yao huku wakijua kuwa maeneo hayo ni ya kwao.
Kauli
ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
wakati akikagua maeneo ya msitu wa kazimzumbwi yaliyoathiriwa na watu
wanaodaiwa kuvamia msitu huo na kuchoma moto kwa madai kuwa maeneo hayo ni ya
kwao.
Nyalandu
amesema kuwa ingawa Wizara hizo zitakaa pamoja ili kurekebisha kasori hizo
lakini ramani ya awali ambayo inatambulika na Wizara ya Maliasili na sio ile
iliyochorwa na Wizara ya ardhi.
Kwa
upande wake Meneja Misitu ya Pugu,Kaimzumbwi na Vikindu Bw.Matthew Mwanuo
amesema mipaka iliyotengwa na Wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ina utata
kufuatia kutoa zaidi ya mita 900 takribani kilomita moja za msitu kuingia katika
makazi ya wananchi wa kijiji cha maguruwe kilichopo Wilaya ya Kisarawe.
Nae
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa huduma za Misitu TFS Bw.Juma Mgoo amesema ni muhimu
Wizara hizo mbili zikasimamia sheria za mipaka na sio kupindisha sheria hatua
inayoweza kusababisha umwagaji wa damu kutokana na kugombania mipaka.
No comments:
Post a Comment