Mahakama ya hakimu mkazi kisutu
imesogeza mbele kesi inayomkabili aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya shirika la
usafiri Dar es salaam UDA Iddi Simba anayekabiliwa na shitaka la matumizi
mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya shilingi Bilion 2.4
Mbali na Simba ambaye aliwahi kuwa
waziri wa viwanda na biashara washtakiwa wengine ni aliyekuwa meneja mkuu
wa UDA Victor Milanzi na mkurugenzi wake Salim mwaking’inda.
Majira ya saa tatu asubuhi ambapo
Idi Simba pamoja na wenzake wamefika katika mahakama ya mkazi kisutu kwa ajili
ya kuanza kusikiliza kesi hiyo ambapo hakimu mfawidhi Ilvin Mgeta ametaja
tarehe 16 ya mwezi august kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo.
Simba pamoja na aliyekuwa meneja wa
mkuu wa wa Uda Victor Milanzi wanakabiliwa na kosa la kughushi barua wakionesha
kuwapo kwa kiwango cha fedha kwenye akaunt zote za benki za Uda fedha ambazo
hazikuwepo wakitenda kosa hilo septemba 2 mwaka 2009.
Siku hiyo hiyo wakakutwa na kosa la
kuchepusha fedha shilingi million 320 wakijifanya ni malipo ya awali ya mauzo
ya Hisa katika shirika hilo fedha ambazo walijipatia kutokana na nyazifa
walizokuwa nazo.
Washitakiwa Simba na Mwaking'inda
kati ya septemba 2009 na FebruarI 2011waliharibu hisa za Milioni 7.8 zisizotumika
na shirika hilo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi Trilion 1.14 bila
kufuata taratibu za zabuni kitendo ambacho ni uvunjaji wa masharti ya kanuni ya
63(1)ya ununuzi ya uma.
Kwa ujumla washtakiwa wote wanadaiwa
kuwa February 11 2011 walishindwa kuchukua tahadhali zinazostahili kwa kumuuzia
kampuni ya simon Group hisa milioni 7.8 zisizotumika kwa bei ya shilingi trilio
1.14 ambapo wangeweza kutoa ofa kwa mnunuzi kununua kwa bei ya juu zaidi na
hivyo kusababisha hasara ya shilingi trillion 2.3 kwa shirika hilo.
Washitakiwa hao walitakiwa kutoa
hati ya nyumba na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kila mmoja asaini
bondi ya shilingi million 500 ambapo Idi Simba aliwasilisha hati ya nyumba
yenye thamani ya shilingi billion8 na kuridhia wenzake waweze kuitumia kupata
dhamana.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa august
16 mwaka huu ambapo washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment