Monday, July 23, 2012

MAANDALIZI YA SIKU YA MASHUJAA YAKAMILIKA

Maandalizi kwa ajili maadhimisho ya siku ya mashujaa nchini yamekamilika ambapo Jumatano hii Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa july 25 kila mwaka ikiwa ni hatua ya kuwakumbuka mashujaa watanzania waliopoteza maisha wakiwa katika harakati za kupigainia uhuru.

Katika viwanja vya mnazi mmoja pembezoni mwa mnara wa mashujaaa, vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vikiwa katika maandalizi ya mwisho ya kujiandaa na maadhimisho ya siku ya mashujaa nchini.

Mbali na gwaride hilo pia siku hiyo kutakuwa na fursa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya kikwete kuweka ngao na mkuki kwenye mnara huo ikiwa ni kuwakumbuka mashujaa hao.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, na hapa ansema kila kitu kimekwenda sawana na kuwataka wananchi kuhudhuria kwa wingi siku hiyo.

Flora Mazeleng’we ni mkurugenzi wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wa Tanzania, hapa anaelezea umuhimu wa mwenge utakaowashwa usiku wa kuamkia siku hiyo.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadik amtoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara za Nyerere, Uhuru na Bibi Titi Mohamed kuwa zitafungwa kwa muda kupisha shughuli hiyo.


No comments:

Post a Comment