Monday, July 23, 2012

KONGAMANO LA KUJADILI MASUALA YA UTALII KUFANYIKA AGOSTI 8 NA 9

Kongamano la kujadili masuala ya utalii kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania linatarajia kufanyika Agosti 8na 9, mwaka huu kisiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kukuza sekta ya utalii nchini.

Kongamano hilo linatarajia kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wakiwemo wanataaluma na watunga sera ili kujadili mbinu za kutafuta masoko na kukabili changamoto zilizopo kwenye sekta ya utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi amesema kuwa bado jitihada za ziada zinahiatajika katika kukuza sekta ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko kwenye sekta hiyo.

Moshingi amesema hayo wakati akikabidhi hundi ya Sh milioni tano kwa Idara ya Masoko ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwaajili ya uratibu wa kongamano hilo.

Amesema umefika wakati kwa watanzania kuendeleza sekta ya utalii bila kutegemea wafadhili kutokana na kutohitaji fedha nyingi kwaajili ya uwekezaji.

Kongamano ni sehemu ya mpango mkakati wa upatikanaji wa mbinu za kuimarisha sekta ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa sera zitakazosaidia kupanua wigo wa sekta hiyo na ongezeko la watalii nchini.

No comments:

Post a Comment