Waziri Tibaijuka akiongea na wakazi wa Manzese |
Mpangilio mbovu wa makazi katika maeneo ya uswahili katika
majiji mbalimbali huenda yakaigharimu serikali katika mpango wake wa kuboresha
makazi unaoratibiwa na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Licha ya kuwepo hali hiyo Waziri wa ardhi Nyumba na
Maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka amewatoa hofu wananchi kuwa
watafanikiwa kwa kufuata mpango wa kuboresha makazi huku wakitafuta namna ya
kuboreha makazi hayo.
Profesa Tibaijuka amewasili katika kata ya Manzese Mvuleni
na kutembelea nyumba kadhaa zilizoanza kuboreshwa katikati mwa kata hiyo yenye
idadi kubwa ya makazi yasiyopangika
Akiwa hapo akatoa ufafanuzi endapo kuna mpango wowote wa
kuyavunja makzi hayo ili kujenga ya kisasa zaidi na akatolea ufafanuzi suala
hilo
Wakazi wa maeneo hayo pamoja na kusifu uamuzi wa Waziri
kufika katika maeneo hayo, wana mapendekezo yao kwa serikali huku wengine
wakiwa na hofu ya kutegemea mkopo katika ujenzi wa makazi yao.
Wizara ya Profesa Tibaijuka bado ina kazi kubwa ya
kuhakikisha wananchi wananeemeka na mradi wa kuboresha nyumba TAFSUS unaofanywa
kwa kushirikiana na Mabenki mbalimbali, na kuhusiana na mlolongo mrefu wa
kupata mkopo huyu hapa ni Bw. Twaha Ally Dima miongoni mwa wakazi waliofaidika
na mpango huo, huku Mkurugenzi wa Benki ya Azania naye akigusia suala hilo
Ziara ya Profes Tibaijuka katika maeneo hayo yenye makazi
duni yatuma ujumbe kwa wananchi kukubali mabadiliko katika makazi chini ya
mkakati ulionzishwa na Waziri huyo wa sasa katika nyumba na makazi wakati akiwa
Katika umoja wa mataifa.
No comments:
Post a Comment