Monday, July 23, 2012

FAO LA KUJITOA KATIKA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII LIMEFUTWA

Irene Isack, Mkurugenzi SSRA
Mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya jamii SSRA Irene Isack  amesema fao la kujitoa limefutwa ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii.

Hilo limetokana na wanachama wengi kutaka kujitoa katika mifuko hiyo na baadae wanapopata matatizo wanataka kurejea tena kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo kwa mfano wafanyakazi wa mgodini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mkurungezi wa SSRA Irene Isack amesema kwa mujibu wa marekebisho hayo mwanachama atapata  mafao yake pale atakapofikisha miaka ya kustaafu kwa hiari miaka 55 na kwa lazima miaka 60.

Nao baadhi ya  wakurugenzi  wa mifuko ya jamii  Crescentius Magori wa NSSF na William Erio wa PPF wamesema kuwa mwanachama anaweza kupata mkopo wa nyumba kupitia michango yao.

Kwa mujibu wa Bi. Irene  mwanachama haruhusiwi kuhama mfuko hata kama akiwa mapumziko na iwapo atarejea atatakiwa kurudi kwenye mfuko wake wa awali na mwanacha mpya ndo anaruhusiwa kuchagua mfuko huku mamlaka ikiwa imeandaa kanuni za mafao ili kuboresha maslahi yao

No comments:

Post a Comment