Tuesday, July 24, 2012

FAUSTIN SUNGURA ALALAMIKIA KUCHELEWESHWA KWA KESI MAHAKAMANI

SUNGURA.JPG
Bw. Faustin Sungura

SUNGURA4.JPG
Bw. Faustin Sungura

Aliyekuwa Mgombea wa ubunge katika jimbo la uchaguzi la Moshi mjini mwaka 2010 kupitia NCCR MAGEUZI-Faustin Sungura amelalamikia Ucheleweshwaji wa kesi unaofanywa na Mahakama kuu kanda ya Moshi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Bw. Sungura dhidi ya mwanasheria mkuu  wa serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Philemon Ndesamburo.

Alipokutana na waandishi wa habari katika makao makuu ya NCCR Mageuzi , Sungura amedai kuwa mazingira ya kuendesha kesi yake yametawaliwa na rushwa huku akimtuhumu jaji Moses Mzuna wa mahakama kuu kanda ya Moshi anayesimamia kesi hiyo  kuhusika katika kukwamisha kesi yake

Madai ya msingi ya kesi hiyo ni kupinga kiasi kikubwa cha dhamana kulingana na mwenendo wa mahakama kuu inayoendesha kesi yake

Pamoja na hayo Bw.Sungura amesisitiza kuwa ukiukwaji wa wazi wa sheria unaofanywa na jaji na kulingana na hali hiyo  amechukua uamuzi wa kuachana na mahakama na kutumia njia za kiutawala

Baadhi ya Ngazi hizo za kitawala ni pamoja na kuandikia barua kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania,jaji mkuu,mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa ,mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa na nyinginezo ili haki iweze kutendeka juu yake. 

Dennis Mwasalanga
  
  
  

No comments:

Post a Comment