Saturday, August 4, 2012

SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO WATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA VIJANA WENYE UJUZI NA VIPAJI

Serikali pamoja na wadau wa maendeleo nchini wametakiwa kutoa kipaumbele kwa vijana wenye ujuzi na vipaji mbalimbali ili kusaidia kuinua vipaji vyao na kujikwamua kiuchumi.
 Wito huo umekuja kufuatia kundi kubwa la vijana wanaomaliza kukosa ajira licha ya kuwa na vipaji kutokana na aidha kukosa fursa za kuajiriwa au mitaji ya kujiajiri wenyewe.

Mwenyekiti mtendaji wa kikundi cha vijana wajasiriamali Twisuka Bibi Mary Mkalawa amesema vijana wa Pwani wana moyo wa kujituma katika kujiendeleza kimaendeleo lakini wamekosa fursa ya kutumia vipaji vyao kwa kukosa mitaji, mikopo na Ruzuku toka serikalini.

Vijana hao wajasiriamali wamesema katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani soko limepungua kutokana na kukosekana kwa wageni .

Serikali pamoja na wadau wa maendeleo nchini wamekuwa wakiungana na makundi ya vijana katika kusaidia kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa ajira nchini.

No comments:

Post a Comment