Saturday, August 4, 2012

RWANDA YAZIDI KUFANIKIWA KATIKA SEKTA YA ELIMU

Dr. Ben Rugangazi - Balozi wa Rwanda Tanzania
Nchi ya Rwanda imeendelea kufanya vizuri katika sekta ya elimu ambapo kufikia sasa imejenga vyuo vikuu 13 kutoka chuo kimoja miaka 12 iliyopita wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mauaji ya kimbari.
Nchi ya Rwanda imefanikiwa kufika hapo baada ya mpango wake wa kutenga asilimia 20 ya fedha katika bajeti yake kwa ajili ya maendeleo ya elimu ikiwa ni pamoja na kwa kujenga vyuo vikuu 13 katika kipindi hicho cha miaka 12.

Hayo yamesemwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dr. Ben Rugangazi wakati akiainisha maswala mbalimbali yanayohusu nchi hiyo mbele ya waandishi wa habari Jijini hapa.

Dr. Rugangazi amesema kuwa ingawa nchi yake imefanya vizuri katika maendeleo ya elimu lakini bado inakabiliwa na changamoto katika miundombinu ya barabra pamoja na uzalishaji wa umeme.

Ameoangeza kuwa katika kuboresha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali, nchi yake ipo katika mazungumzo na serikali ya Tanzania na zambia kwa lengo la kuunganisha reli kutoka Zambia mpaka Tanzania.

Nchi ya Rwanda ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 12 kwa utegemezi wa kilimo na utalii ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita iliondoa kibali cha kuingia nchini humo pamoja kibali cha ufanyaji wa kazi kwa Raia wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment