Saturday, August 4, 2012

WAISLAM WAASWA KUUTUMIA VIZURI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Alhaji Musa Saluum - Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhadji Musa Salum amewataka waisilamu nchini kote kuutumia vizuri mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumrudia Mwenyezi Mungu na kuachana na yale yaliokinyume na imani ya dini yao

Alhaji Musa salum amesema katika mahojiano maalumu na Star tv ofisini kwake, kuhusiana na umuhimu wa kutekeleza nguzo ya kufunga hasa ikizingatiwa kuwa leo ni Ramadhani 15.

Akieleza umuhimu wa mwezi wa Ramadhani Alhaji Musa Salum emesema kipindi hiki cha mfungo kitawasaidia kuimarisha imani zao

Alhaji musa Salum aefafanua kuwa bado kuna haja ya kuimarisha imani ili kushinda changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa maadili

Pia ameeleza kwamba siku hizi watu wengi hawana ushirikiano katika kufungua tofauti na zamani ambapo walikuwa wanaungana pamoja wakatiwa jioni wanapofuturu

No comments:

Post a Comment