Saturday, August 4, 2012

ATCL YASITISHA SAFARI ZA DAR-MWANZA KUPITIA KILIMANJARO








Shirika la ndege la Tanzania ATCL limesitisha kwa muda safari zake za kutoka dar es salaam kwenda mwanza kupitia kilimanjaro kutokana na kusitishwa kwa mkataba wa ndege ya air boeing 737/500

Ndege hiyo iliyokodiwa mwezi wa tano mwaka huu kutoka kampuni ya aero vista ya nchini dubai mkataba wake umekuwa na utata na kulazimu kusitishwa kutoa huduma ili kupisha nafasi ya mazungumzo ya kurekebisha vipengele vyote vyenye utata.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkurugenzi wa shirika la ndege kapten Milton Lazaro amesema wamefanya hivyo kutokana na sababu zisizozuilika huku wateja wao wakiendelea kupata huduma kupitia makampuni wanayoshirikiana nayo.

No comments:

Post a Comment