Monday, June 18, 2012

Ogunde kuzikwa Serengeti

Marehemu Willy Ogunde (Picha kutoka in2eastafrica.net)
Mwili wa aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo unatarajiwa kuzikwa juma tano Serengeti, mkoani mara. Willy Ogunde alifariki usiku wa kuamkia jana mjini Morogoro alipokwenda kwa mkutano wa siku moja uliohusu sensa ya watu na makazi ulioandaliwa na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS). Kifo chake kilikuwa cha ghafla alipoanguka chini ghafla na kupelekwa hospitali. Gazeti la Majira lilibaini kwamba marehemu alipofikishwa hospitali alikuwa tayari amefariki baada ya vipimo vya daktari. Mbali na matatizo yake ya moyo aligonga kisogo chini alipoanguka. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi

No comments:

Post a Comment