JUMUIYA ya Madaktari
Tanzania imetangaza kuanza rasmi mgomo usio na kikomo kwa nchi nzima June 23,
mwaka huu mpaka serikali itakapotoa ufumbuzi wa kutatua madai yao
yaliyowasilishwa serikalini Januari 27, mwaka huu.
Awali madaktari hao
walitoa muda wa wiki mbili kwa serikali kuhakikisha inatimiza madai yao ambapo
hadi sasa wamesema hakuna ufumbuzi wa madai yoyote yaliyofanyiwa kazi licha ya
kukaa meza moja na serikali na kukubaliana kutatuliwa kero zao.
No comments:
Post a Comment