Thursday, July 26, 2012

MELI TATU ZAFUNGIWA ZANZIBAR


Uokoaji baada ya Ferry ya MV Skagit kuzama
Serikali ya Zanzibar imefuta usajili wa meli tatu ikiwa ni mojawapo ya jitihada ya serikali hiyo kupunguza visa vya ajali za baharini.

Serikali pia imeliagiza mamlaka ya kusimamia usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA kuongeza utendaji kazi wake hadi Zanzibar
Hatua hii inakuja wiki moja baada ya meli ya MV Skagit kuzama baharini wakati ikielekea zanzibar.

Miongoni mwa meli hizo zilizoharamishwa ni MV Kalama ambayo pia inamilikiwa na wenye MV Skagit.
Katika ajali hiyo watu zaidi ya 150 walikufa maji.

Hii nikuja siku moja tu baada ya Serikali ya Tanzania kuagiza SUMATRA kufanya kazi yake ipaswavyo.
Katika agizo lake Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais Mohammed Aboud amesema SUMATRA lazima ikague meli zote za Zanzibar kuangalia kama zinastahili kuwa baharini au la.

No comments:

Post a Comment