Thursday, July 5, 2012

RUBADA YASAINI MAKUBALIANO YA AWALI YA KUZALISHA UMEME


Aloyce Masanja – Mkurugenzi - RUBADA

Francisco Luz – Barozi wa Brazil




Mamlaka ya uendeshaji wa bonde la mto Rufiji RUBADA umesaini mkataba wa makubaliano ya awali ya kuzalisha nishati ya umeme kupitia mradi wa stiegler’s Gorge na kampuni ya Odebretch Group ya Brazil

Mkataba wa makubaliano ya mradi huo umesainiwa jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa RUBADA Aloyce Masanja na mkurugenzi wa biashara wa Odebretch Fernando Soares.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo  mkurugenzi wa RUBADA Aloyce Masanja amesema mradi  huo uko katika hatua muhimu na ukikamilika utaleta manufaa makubwa ya kibiashara na kiuchumi kwa taifa

Francisco Luiz ni Balozi wa Brazil hapa nchini amesema mradi huo ni chachu katika kuchochea kasi ya maendeleo ya nishati hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo na kupunguzia adha ya kukosekana kwa umeme.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya uendeshaji wa bonde hilo Profesa Raphael Mwalyosi amesema wanategemea serikali itasimamia na kuhakikisha mradi huo wa stiegler’s Gorge unakamilika kwa wakati

Makubaliano hayo yanatoa fursa ya kuanza kufanyika kwa upembuzi yakinifu kupitia ule uliofanywa awali na Norway mwaka 1980 na kufanyika maboresho ambapo baada ya miezi 6 kampuni hiyo itatoa ripoti ya kwanza itakayoonyesha mda wa kuanza na kumalizika kwa mradi huo.

No comments:

Post a Comment