Tuesday, July 3, 2012

MNYIKA APEWA SIKU 7 KUTHIBITISHA KUWA MWIGULU NCHEMBA NI MMOJA WA WATUHUMIWA WA EPA

Mh. John Mnyika, Mbunge wa Ubungo

Leo bungeni Mh. John Mnyika, mbunge wa Ubungo (CHADEMA) amepewa siku saba kuwasilisha ushahidi unaothibitisha kuwa Mh. Mwigulu Nchemba Lameck ni mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya EPA.

Hayo yametokea wakati Mh. Mnyika akichangia hoja katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya ofisi ya rais na kumshutumu Mh. Nchemba kuwa naye ni mmoja ya watuhumiwa wa EPA kwa kuwa aliwahi kufanya kazi benki kuu na pia ni mhasibu wa CCM.

Nae Mh. Mwigulu Nchemba ametoa utangulizi juu ya hilo na kusema mwaka 2006 wakati ufisadi wa EPA umetokea yeye alikuwa bado chuoni na hakuwa mtumishi wa benki kuu. Kwa hiyo Mnyika anayo kazi ya kuthibitisha hizo shutuma.

No comments:

Post a Comment