Clemence Masanja, Mwenyekiti Chama Cha Maderva wa Malori Tanzania |
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori Tanzania,Bw. Clemence Masanja ameiomba serikali kuingilia swala la maderera 12 wa malori ya mafuta ya kampuni ya DANDHO waliokamatwa na kufungwa jela nchini Zambia kwa madai ya kuchakachua mafuta.
Bw. Masanja amedai kuwa watanzania hao wanateseka kwa kuonewa na wanaiomba serikali iingilie na kuwasaidia kwa kupitia mahusiano ya kidiplomasia yaliyopo kati ya Tanzania na Zambia.
Madereva hao walikamatwa wakiwa 14 na wawili walifanikiwa kutoroka wakati wakipeleka mafuta ya katika mji wa Ndola nchini Zambia.
No comments:
Post a Comment