![]() |
Panji Kaunda, Naibu Waziri wa Uchukuzi Zambia |
![]() |
Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria mkutano huo |
![]() |
Baadhi ya wafanyabiashara walioudhuria mkutano huo |
Serikali
ya Zambia imetenga jumla ya Dola Milioni 10 kwa ajili ya uboreshaji wa
Shirika la Reli ya Tazara pamoja na changamoto mbalimbali zinazolikabili
shirika hilo.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Bwana Panji Kaunda amethibitisha hilo leo jijini
Dar es salaam wakati akifungua mkutano mkuu kati ya wafanyakazi wa Shirika hilo
na Wafanyabiashara wakubwa wanaosafirisha bidhaa zao kwa kutumia Reli ya
Tazara.
Waziri Kaunda amesema pia kuwa ni wajibu wa serikali zote mbili kati ya
Tanzania na Zambia kuboresha mahusiano mazuri kwa kuwekeza katika shirika hilo
ili kuwavutia wafanyabiashara kuendelea kusafirisha bidhaa zao na hatimaye
kukuza uchumi wa nchi hizo.
Naye
katibu wa wizara ya uchukuzi nchini Tanzania Bwana Omary Chambo amesema hii ni
mara ya kwanza kwa nchi ya Zambia kutenga bajeti kwa ajili ya shirika hilo. Nao
baadhi ya wafanyabiaashara wamezitaka nchi zote mbili Tanzania na Zambia
kuboresha miundombinu ya shirika hilo ikiwemo mishahara ya wafanyakazi ili
kupunguza migogoro baina ya wafanyakazi na Serikali.
No comments:
Post a Comment