![]() |
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu |
Tatizo
la mimba mashuleni kwa Wakazi wa Kata ya
Songwa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga linadaiwa kuathiri kiwango cha elimu
kwa watoto wa kike kutokana na umaskini katika maeneo wanayoishi.
Bi Rachel Mdundo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP ngazi ya Jamii amesema kuwa
utafiti uliofanywa katika kipindi cha mwaka 2011 pekee umebaini kuwa wanafunzi 31 wa
kata ya Songwa wamepata ujauzito na kusababisha kukatiza masomo yao.
Naye
Bi Jamila Nyalulu ambaye ni mmoja wa wazazi katika Wilaya hiyo anasema kumekuwapo na
tabia za wazazi kuwaamuru watoto kutofanya vizuri makusudi katika mitihani yao
ili wafeli kwa kigezo cha kuwasaidia kazi za nyumbani hatua inayodidimiza sekta
ya elimu wilayani hapo; kauli ambayo inaungwa mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu Injinia Lucas Said ambaye anasema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa
wanafunzi kuhusiana na hatua hiyo na kuahidi kulifanyia uchunguzi suala hilo
ili sheria ishike mkondo wake.
Kumekuwa
na chamgamoto mbalimbali zinazohusu elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu mojawapo ikiwa ni mimba mashuleni,vifaa vya kufundishia,nyumba za
walimu na mengine mengi,jitihada za haraka zinahitajika ili kuweza kuinusuru
hali hiyo.
No comments:
Post a Comment