Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania |
Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia |
Dr. Hussein Mwinnyi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii |
Rais Kikwete na Rais Sirleaf wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi za ALMA Dar es Salaam |
Rais wa Liberia na mwenyekiti wa umoja wa ushirikiano wa
viongozi wa afrika unaoshugulikia Ugonjwa wa malaria ALMA Ellen Johnson Sirleaf
amesema kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kuweka mkazo katika vita dhidi ya
malaria ili kuondokana na maambukizi ya ugonjwa wa malaria.
Rais Sirleaf ameyasema hayo jijini dar es salaam wakati akifanya
uzinduzi wa ofisi ya ALMA ambayo itashughulikia kwa kiasi kikubwa kuweka
mikakati ya kutokomeza ugonjwa wa malaria.
Mpaka kufikia sasa vyandarua million 400 vimegaiwa kwa nchi
zilizopo kusini mwa jangwa la sahara ambapo Tanzania ilipata vyandarua million
17 kwa wanawake wajawazito pamoja na vyandarua million 9 kwa watoto wenye umri
chini ya miaka 5 vilivyotolewa bure kwa lengo la kupunguza maambukizi.
Naye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
amesema kuwa Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa
malaria kwa kipindi cha miaka3 na Zanzibar wamefanikia kuondoa ingawa
wanahitaji kujiridhisha kwa kuongeza nguvu Tanzania bara ili kuondokana na
maambukizi yatakayosambaa.
Naye waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr.hussen Mwinyi amesema
kuwa dawa ya mseto dozi ya malaria kwa mtu mzima inatakiwa kuuzwa kwa shilingi
1600 kutokana na kuwa na ufadhili wa global fund ambao unapelekea kuuzwa kwa
dawa hiyo kwa bei ya chini.
Nchi za Afrika ndizo zinaongoza kuwa na magonjwa wa malaria kwa
asilimia 83 ambapo vifo vinavyotokana na maradhi ya malaria ni asilimia 89
ambayo kwa kiasi kikubwa vinatokana na wananchi wanaoshindwa kununua vyandarua
pamoja na dawa.
Umoja wa ushirikiano wa viongozi wa afrika unaoshughulikia
utokomezaji wa ugonjwa wa malaria ALMA ulianzishwa mwaka 2009 newyork marekani
ambapo Rais kikwete alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza.
No comments:
Post a Comment