Imeelezwa kuwa mfumuko wa bei za bidhaa na kupanda kwa bei za
vyakula hapa nchini ni matokeo ya matumizi makubwa ya serikali yasiyo na tija
kwa wananchi na kusababisha kutengwa kwa bajeti ndogo katika masuala ya
maendeleo.
Hayo yamebainishwa jijijni Dar es salaam na Mwenyekiti wa chama
cha wananchi CUF ambaye pia ni mtaalam wa uchumi ambapo amesema matumizi
ya serikali yameongezeka kutoka trioni 13.1 mpaka trilioni 15.1.
Kwa upande wa baadhi ya wafanyabiashara wa nafaka katika soko la
Buguruni jijini Dar es salaam wamesema kupanda kwa bei za mafuta na umeme ni
sababu kubwa inayochangia kutoshuka kwa bei za vyakula hata katika kipindi hiki
cha msimu wa mazao.
Amesema ili kupunguza gharama za maisha ni lazima uzalishaji
uongezeke lakini sekta ya kilimo haijatengewa fedha za kutosha kwa madhumuni ya
kuongeza tija ya uzalishaji wa chakula na mazao mengine ya kilimo
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya uchumi wa taifa inaonyesha kuwa
kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopota sekta ya kilimo, misitu na uvuvi
zimekuwa zikitengewa chini ya asilimia 5 ya matumizi yote ya serikali.
Kwa mujibu wa makubaliano ya nchi za SADC ni kutenga
angalau asilimia 10 ya matumizi ya serikali katika sekta ya kilimo ili kuongeza
kasi ya ukuaji wa sekta hiyo kwa kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza
umaskini uliokithiri
No comments:
Post a Comment