Samson Majwala-Meneja wa Nokia |
Katika kipindi hiki cha KUELEKEA Mwezi mtukufu wa
Ramadhani Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania imeingia ubia na
kampuni ya Nokia na kurahisisha upatikanaji wa Quran kwenye simu ya mikononi.
Meneja wa Nokia hapa nchini Samson Majwala ameelezea uzinduzi wa
huduma huo kuwa utajumuisha ofa ya simu za Nokia Asha 200 na Nokia
Asha 302.
Ushirikiano huo baina ya Vodacom na Nokia pia umewalenga vijana
wengi pamoja na wafanyakazi wote wenye matumizi makubwa ya mitandao ya
kijamii Facebook. Twitter pamoja na Wikipedia ofa ambayo itadumu miezi sita.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Bidhaa kutoka Vodacom Mgopelinyi
Kiwanga amewaambia wateja wao kuwa huo ni mfululizo wa kuileta jamii karibu
zaidi katika mawasiliano hususani ya mtandao wa internet.
Ushirikiano baina ya Nokia na Vodacom huenda ukafanikisha
kumaliza kero za mawasiliano hapa nchini.
No comments:
Post a Comment