Shirika la umeme Tanzania TANESCO linatarajia
kuongeza megawatt 100 kwenye grid ya taifa baada ya kukamilika kwa mtambo wa
kuzalisha umme kwa kutumia mafuta.
Kukamilika kwa mtambo huo uliojengwa kwa fedha
za serikali kutaongeza megawatt za umme kwenye grid mpaka kufikia 800 na hatimaye kupunguza tatizo la mgao wa umeme.
Badra Masoud ambaye ni meneja uhusiano wa TANESCO amesema tayari wamelipa deni la Songas na kuongeza pia kuwa moja ya vipaumbele vilivyowekwa katika bajeti ya mwaka
2012/2013 ni uimarishaji wa miundombinu ya nishati ya umeme ili kuweza
kuzalisha zaidi pamoja na kupunguza kupanda kwa gharama ya maisha kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment