Sunday, July 1, 2012

Nanyaro aagwa kwa gwaride maalum

Agustino Nanyaro akiwapungia waliofika kumwaga katka viwanja vya chuo cha maofisa wa jeshi la magereza

Nanyaro akiongea na waandishi wa habari



Nanyaro akiwa katika gari maalum

Askari magereza

Askari magereza wakipiga gwaride


Gwaride maalumu lilitoa heshima kwa kamishna Generali wa Magereza Augustino Nanyaro ambaye amestaafu kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma jana katika viwanja vya chuo cha maofisa wa jeshi la magereza Ukonga.

Makamanda wa Magereza walihitimisha utumishi wa Bw. Nanyaro kwa kusukuma gari maalumu lililoandaliwa kwa shughuli hiyo mpaka nje ya geti.

Aidha bw. Nanyaro amesema nidhamu, uadilifu na kufanyaji kazi kwa bidii ndio njia pekee ya kuliwezesha jeshi hilo kufanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa.
Nanyaro amabye amelitumikia jeshi la Magereza kwa zaidi ya miaka 37 amestaafu wadhifa huo huku akiwa amefanya mabadiliko kadhaa ikiwa ni pamoja na kulifanya jeshi hilo kufanya kazi zake kisasa zaidi.

No comments:

Post a Comment