Sunday, July 1, 2012

Pinda awataka wajasiriamali kutumia barcode



Dr. Mary Nagu

Pinda na Nagu wakiangalia bidhaa mbalimbali

Bidhaa za nguo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda


Waziri mkuu Mizengo pinda amewataka wajasiriamali nchini kuwa na mikakati ya kupanua wigo wa biasahara zao nchini  na nje ya nchi kwa kufuata utaratibu wa kubandika stempu za barcodes katika bidhaa zao.
Akisisitiza ubora wa bidhaaa za viwanda vidogovidogo nchini Waziri Mkuu amewataka wajasiriamali hao kuzingatia upitishaji wa bidhaa zao katika shirika la viwango TBS ili kuhakikisha viwango vya bidhaa zao.
Pinda ameyasema hayo wakati wa sherehe za utoaji ruzuku kwa wajasiriamali 870  waliopatiwa msaada huo chini ya mpango wa kuinua wajasiriamali wa BDG. Pia amesema serikali imeazimia katika bajeti ya mwaka huu wa fedha kuondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ikiwa ni jitihada za kukuza viwanda vya nguo nchini.
Nae  waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu amesema kuwa ili kuvutia uwekezaji kwa wazalendo na wageni serikali ni lazima iangalie sera na sheria katika kumtengenezea mwekezaji mazingira mazuri

Zaidi ya shilingi bilioni 5 zimegawiwa kwa wajasiriamali kote nchini kupitia mradi wa ushindani wa faidika kibiashara BDG unaofadhiliwa na serikali ya Uingereza na kuratibiwa na taasisi ya sekta binafsi nchini – TPSF.

No comments:

Post a Comment