Sunday, July 1, 2012

Dr. Ulimboka apelekwa nje ya nchi kwa matibabu

Dr. Steven Ulimboka baada ya kutekwa na kupigwa

Dr. Steven Ulimboka kabla ya kutekwa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk Stephen Ulimboka amesafirishwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu zaidi kufuatia hali yake kuzidi kuwa 
mbaya.

Dk Ulimboka ambaye awali alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu ICU katika Taasisi ya Mifupa MOI amesafirishwa jana kwenda  nchi ambayo wahusika wamekataa kuitaja japo inatajwa na magazeti na vyombo vingine vya habari kuwa India na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment