Saturday, June 30, 2012

Walimu wasusia semina

Baadhi ya walimu waliohudhuria semina hiyo

Baadhi ya walimu waliohudhuria semina hiyo

Bernard Mkali, Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam

Baadhi ya walimu waliohudhuria semina hiyo



Walimu wa masomo ya sayansi mkoa wa Dar es salaam wamesusia semina ya kitaifa ya mafunzo kwa vitendo, wakipinga posho  ya shilingi 15000, wanayolipwa kwa siku, kwa madai kuwa hailingani na maisha ya jijini Dar es salaam.

Semina hiyo ambayo inayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara inafanyika Jijini Dar es salaam kwa siku kumi na sasa inatishiwa kuvunjika kutokana na udogo wa posho.

Haikuwa kazi rahisi kuwatuliza walimu hawa ambao madai yao ya msingi yalielekezwa  kwenye upande wa maslahi kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa jijini humu.

Walimu hawa kwa mujibu wa madai yao ambayo yanazingatia waraka namba 1 wa  mwaka 2005 ulioweka viwango vya posho ya kujikimu kwa safari za kikazi ndani ya nchi ambavyo vilianza kutumika mwaka 2008 na kuendelea hadi sasa wanadai wanapaswa kulipwa shilingi 45,000 kwa siku.

Kikubwa ni kwamba Bw. Bernard Makali ambaye ni Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam na kaimu katibu tawala wa mkoa huu anakanusha madai hayo na kusema mwongozo hakuna mahali katika mwongozo unaosema walipwe posho ya 45000.

No comments:

Post a Comment