Geti la hospitali ya Muhimbili |
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri huduma bila mafanikio |
Mmoja wa wagonjwa waliofika hospitalini hapo |
Siku
moja baada ya Serikali kushindwa kutoa msimamo wake kuhusiana na mgomo wa
madaktari unaoendelea nchi nzima utoaji wa huduma katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili umesimama kufuatia mgomo huo.
June
27, mwaka huu bungeni mjini Dodoma Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitangaza kutoa
tamko kuhusiana na mgomo huo siku inayofuatia
ambapo hali ilikuwa tofauti baada ya msimamo huo kushindwa kutolewa.
Kufuatia
hali hiyo baadhi ya wananchi na wagonjwa waliofika hospitalini hapo wameishauri
serikali kukaa meza moja na madaktari ili kupata suluhisho la mgogoro huo
kutokana na kuwaathiri watanzania wengi hususani wenye kipato cha chini.
Juni
21, mwaka huu Jumuiya ya Madaktari Tanzania ilitangaza kuanza kwa mgomo rasmi
wa madaktari usio na kikomo nchi nzima hadi serikali itakapoanza kutatua madai
yao yaliyowasilishwa serikalini Januari 27, mwaka huu ambapo miongoni mwa madai
hayo ni pamoja na uboreshwaji wa mazingira ya kufanyia kazi na nyongeza ya
posho na mishahara.
No comments:
Post a Comment