Said Meck Sadick, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam |
Gari lenye mtambo maalum wa kuzolea taka |
Jiji la Dar es Salaam limeanza mkakati wa kukusanya taka kwa kutumia mitambo maalum ya kuzoa taka na hata kuzisaga pamoja na kusafisha maeneo hayo ili kuboresha hali ya usafi katika jiji hilo. Jiji hilo limekuwa kati ya mikoa yote likiongoza kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na ongezeko la watu
kwenye Jiji hilo.
Maeneo yanayoonekana kuwa machafu kwa wingi ni pamoja na
vituo vya mabasi pamoja na maeneo ya masoko ambayo mara nyingi
yanaonekana kushindwa kufanyiwa kazi kikamilifu hivyo kufanya jiji hilo
kuendelea kuchafuka.
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Said Meck Sadick amekiri kuwepo na uchafuzi huo lakini anasema
kuwa ni jukumu la kila mwananchi kukusanya takataka katika sehemu
zinazotakiwa pamoja na kuzilipia kama ambavyo sheria za serikali ya mitaa
zinavyoagiza.
Kampuni tatu za kutoa huduma za usafi zimepewa tenda katika
manispaa ya Ilala ili kuboresha hali ya usafi hasa katika maeneo ya
vituo vya mabasi pamoja na masokoni hasa
soko kuu la samaki la kimataifa Kivukoni.
No comments:
Post a Comment