Saturday, June 30, 2012

Serikali kuongeza kasi ya kulipa madeni ya PSPF

Eng.Charles Kitwanga-Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais

Lila Mkila-Naibu Gavana-BOT

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo



Serikali  imeahidi kuongeza kasi katika ulipaji wa deni lake kwa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma PSPF ili kufanikisha azma ya ulipaji wa mafao kwa wanachama wake kwa muda muafaka

Mpaka sasa PSPF inaidai serikali shilingi bilioni 716 zinazotokana na mikopo ya serikali kwenye mfuko huo.

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa  Rais Eng Charles Kitwanga akizungumza kwa niaba ya Makamu Wa Rais jijini Dar es Salaam  wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa mfuko huo amesema kuwa serikali inatambua mchango wa mfuko huo katika kutekeleza azma ya kuwapatia wananchi maisha bora hata baada ya kustaafu

Eng. Kitwanga amesema pia kuwa katika kuendeleza sekta ya hifadhi za jamii serikali imeweka mikakati ya ulipaji wa madeni yake kwa mfuko huo ikiwa ni pamoja na kuzihusisha sekta zisizo rasmi ili wananchi katika sekta hiyo waweze kufaidika pia

Naibu gavana wa Benki kuu ya Tanzania bwana Lila Mkila anataja anasema ucheleweshwaji wa fedha zilizowekezwa na mifuko hiyo unachelewesha ulipaji wa pensheni kwa wastaafu ambao ni wanachama wa mifuko hiyo.

PSPF imeweza kuongeza mtaji kutoka biliono 36.4 kwa mwaka 2002 kufikia bilioni 994.4 kwa mwaka 2011 ukiwa na zaidi ya wanachama zaidi ya laki 3 nchi nzima

No comments:

Post a Comment