Pereira Ame Silima Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani |
ACP Charles Kenyela |
Mkazi wa Kigogo akiwatangazia watu waache kunywa gongo |
Kamanda Kenyela akimtuza sh. 5000 mkazi huyo baada ya kutoa matangazo |
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Ame Silima amesema
serikali inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha vifo zaidi ya kumi vya
wakazi wa Kigogo Mbuyuni Jijini Dar es salaam wanaosadikiwa kunywa pombe haramu
ya Gongo inayosadikiwa kuchanganywa na Spiriti na dawa ya Jiki.
Hata hivyo chanzo kamili cha vifo hivyo kinatarajiwa
kujulikana baada ya majibu ya mkemia mkuu wa serikali anayechunguza pombe hiyo.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo la kigogo Mbuyuni Naibu
waziri Silima amewataka watanzania kuachana na tabia ya kuchanganya vitu bila
utaalamu ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni Kamishna
msaidizi wa Polisi Charles Kenyela tangu kutokea kwa tukio hilo wamefanya
oparesheni na kufanikiwa kukamata lita 180 za Gongo na watuhumiwa 12 katika
eneo hilo la Kigogo.
Mwanzo mwa wiki hii watu zaidi ya kumi wamefariki dunia
kwenye eneo la kigogo mbuyuni baada ya kunywa pombe haramu ya gongo ambayo
inadhaniwa kuchanganywa na sumu na wengine 7 bado wamelazwa kwenye hospitali ya
Rufaa ya Amana.
No comments:
Post a Comment