Prof. Ibrahim Lipumba Mwenyekiti CUF |
Mwenyekiyi wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba
amesema kuwa serikali inahitaji kuunda tume huru ya uchaguzi na kuachana na
kutegemea tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni ya uundwaji wa katiba ambayo
itachelewa kumaliza kazi zake kulingana na hadidu za rejea walizopewa.
Prof Lipumba ameyasema hayo katika kikao cha baraza kuu la
chama hicho ambacho kinafanyika kwa siku mbili jijini dar es salaam.
Prof. Lipumba anasema kuwa muda wa kutafuta katiba mpya ni
mfupi na hivyo ni afadhali serikali ikaelekeza nguvu zake katika uundaji wa
tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na uwezo wa kusimamia taratibu na kutoa
takwimu sahihi za wapiga kura kote nchini.
Hata hivyo Prof Lipumba ameongeza kuwa swala la uongezaji wa
fedha za bajeti kutoka shilingi Trilion 13 mwaka 2011/2012 na kufikia shilingi
trillion 15 kwa mwaka 2012/2013 ni kazi bure kwani fedha za maendeleo bado ni
kidogo kulinganisha na mahitaji ya watanzania.
Ameongeza kuwa mfumuko wa bei pamoja na kupanda kwa gharama
za maisha kunatokana na matumizi makubwa ya serikali na pia serikali kushindwa
kutenga asilimia 10%ya bajeti katika kilimo kama ambavyo nchi za SADC
zimekubaliana.
Katika kipindi cha siku mbili baraza hilo litapata nafasi ya
kujadili agenda 10 likiwemo swala la migomo ya madaktari ambao inaonekana
kuathiri kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma za afya kwa watanzania na hasa
wa kipato cha chini.
No comments:
Post a Comment