Saturday, July 14, 2012

WABUNGE WATAKIWA KUTOA ELIMU MAJIMBONI MWAO KUHUSU MFUKO WA BIMA YA AFYA

Jengo la NHIF Dar es Salaam

Dr. Hussein Mwinyi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Baadhi ya waudhuriaji katika mafunzo hayo

Baadhi ya waudhuriaji katika mafunzo hayo

Baadhi ya waudhuriaji katika mafunzo hayo

Baadhi ya waudhuriaji katika mafunzo hayo

Dr. Kebwe Stephen Kebwe Mbunge wa Serengeti



Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye idadi ndogo ya wananchi waliojiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya afya ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ina wanachama wasiozidi milioni 3.5

Kufuatia hali hiyo wajumbe wa kamati ya bunge ya huduma za jamii imewataka wabunge kutoa elimu kwa wananchi kwenye majimbo yao ili wajiunge na mfuko huo.

Tangu kuanzishwa kwake chini ya sheria namba 8 ya mwaka 1999 NHIF imeweza kuwasaidia watanzania kwa asilimia 21 ambayo ni ndogo ikilinganishwa na nchi jirani kama Rwanda ambayo imefanikiwa kwa asilimia 91.

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr. Hussein  Mwinyi ni miongoni mwa viongozi waliofika katika mafunzo yaliyoandaliwa na mfuko huo jijini Dar es salaam na kutambua kuwa idadi kubwa ya wananchi wa kipato cha kawaida hawajajiunga na mfuko huo.

Katika mafunzo hayo kamati hiyo ya kudumu ya bunge imepewa maelekezo mbalimbali ya namna ya utendaji kazi huku wakiachwa na deni la kuwaeleza na kuwasaidia wananchi kufahamu huduma zinazotolewa na NHIF.

Licha ya takwimu za wanaopata huduma za afya kuwa chini Dr. Kwebe Stephen Kebwe ambaye ni  Mbunge wa Serengeti na mwanakamati wa muda mrefu  wa mfuko huo anaona kwamba Tanzania bado ina nafasi ya kuboresha afya za wananchi wake hasa wasiokuwa na kipato cha juu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi  mkuu wa mfuko huo Bw. Emmanuel Humba ikiwa tayari umetimiza miaka kumi, watanzania wengi zaidi watafikiwa kwa asilimia 45 ikiwa ni utekelezaji wa  dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania.

No comments:

Post a Comment