Monday, July 16, 2012

KANISA LA UFUFUO LAMKANA ALIYEDAIWA KUMTEKA DR. ULIMBOKA

Dk. Steven Ulimboka

Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amekanusha taarifa zilizotelewa juzi na kamishna wa polisi kanda maalum Suleiman Kova kuwa bwana Joshua Mulundi raia wa Kenya anayedaiwa kumteka na kutaka kumuua mwenyekiti wa Jumwiya ya madaktari Dk. Steven Ulimboka tarehe 26 Juni alikwenda kanisani hapo kutaka kutubu kosa hilo. Mchungaji huyo ambaye kiongozi wa kiroho katika kanisa hilo alisema kuwa Joshua alitaka kumwona tarehe 27 walipokuwa wakimwombea Dk. Ulimboka lakini walinzi wake walimzuia na akawaambia kuwa yeye ndiye aliyehusika na utekaji wa Dk. Ulimboka hivyo walinzi hao wakampeleka kituo cha polisi. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na polisi mtuhumiwa huyo alisema kuwa anapepo la kuropoka.


Mchungaji huyo kupitia kituo cha televisheni cha Star TV alisema kitendo cha jeshi la polisi kutangazo kuwa Joshua alienda kanisani hapo kutubu si kweli kwa kuwa kanisa hilo halina utaratibu wa watu kutubu na kuanikwa hadharani; hizo ni njama za kulichafua kanisa hilo na waumini wake. Na pia amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwanza kamanda Hemedi Msangi kwa kuwa kuna habari zimeenea kwamba alihusika na sakata la Dk. Ulimboka.


Hivi sasa Dk. Ulimboka yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu na anaendelea vizuri. Ameshaanza mazoezi ya kutembea mwenyewe.

No comments:

Post a Comment