CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimesema kitawachukulia hatua kali za
kisheria baadhi ya wanachama wake wanaosababisha msuguano ndani ya chama
hicho.
CCM imetoa kauli hiyo baada ya uwepo kwa Taarifa kuwa ziara
zinazofanywa na chama hicho hazina baraka za kichama na kwamba hazitambuliki na
Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilson Mukama hali inayozua mkanganyiko kwa
wanachama wake.
CCM imekuwa ikifanya ziara za kichama inayofahamika kama Ziara
ya Ahadi ni Deni kwa kuambatana na watendaji wake kwenye mikoa mbalimbali ya
Tanzania ikiwa ni sehemu ya mipango mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa
kutatua changamoto zinazokwamisha suala zima la kimaendeleo.
Kufuatia ziara za chama hicho ndipo unaibuka mkanganyiko kwa
baadhi ya wanachama wake kudai kuwa fedha za ziara hizo zimetolewa na
Mwenyekiti wa Chama hicho kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye jambo linalomsukuma Nape kutoa kauli hiyo.
Nnauye amesema kuwa ziara hiyo inafahamika kiutawala na kwamba
inabaraka zote za kichama na kubainisha kuwa watu hao wanalengo la
kukidhoofisha chama hicho.
CCM imekwisha fanya ziara
kwenye mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Kagera, Rukwa, Katavi ambapo kesho
inatajia kufanyika Mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment