Monday, June 25, 2012

Wabunge, tumieni nafasi za kuchangia bungeni kuwasilisha matatizo ya wapiga kura wenu

Deus Kibamba, Mwenyekiti Jukwaa la Katiba

William Malecela

Imeonekana katika bunge la bajeti ya 2012/13 kuwa wabunge wengi hawakutumia nafasi zao za kuchangia bungeni vema na badala yake kutoa salamu nyingi, lugha za 'mipasho', na kuongea mambo nje ya mada.

Deus Kibamba, mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba amefafanua kuwa Ibara ya 100 ya katiba inampa mbunge kinga ya kusema lolote lakini wasiitumie kinga hiyo kuongea mambo nje ya mada, lugha za matusi au kukashifiana bungeni.

Hayo yote hufuatia uchambuzi wa kauli ya Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika kwamba hali ya sasa inatokana na 'udhaifu wa Rais, uzembe wa bunge na upuuzi wa CCM' iliyozua mijadala mingi. William Malecela ambaye ni kada wa CCM anasema Mh. Mnyika angeweza kumwambia rais kuhusu huo 'udhaifu' moja kwa moja alipokwenda Ikulu badala ya kuyasema bungeni.

No comments:

Post a Comment