Sunday, June 24, 2012

Simbachawene: Sijafumaniwa

Mh. George Simbachawene (Picha kutoka mjengwablog)

Baada ya habari kutoka mtandao wa kijamii wa Jamii Forum kwamba naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene alifumaniwa na mke wa afisa mmoja wa polisi mkoani Singida na kujeruhiwa kwa panga na mwenye mke huyo kuenea naibu waziri huyo amekanusha madai hayo na kusema ni propaganda za kumchafua.

Katika mazungumzo na kituo cha redio cha Clouds FM jana Waziri huyo alikanusha uvumi huo na kuhisi kwamba ni mpango wa watu wa Chadema wa kumchafua maana watu pekee aliokutana nao hapo Singida na kuwaeleza kuhusu safari yake ya Karatu kwenye msiba ni wabunge wa Chadema waliokuwa wakitokea Tabora.

Pia katika mazungumzo hayo amewaakikishia wananchi kwamba hajajeruhiwa na ni mzima kabisa na kwamba yeye ni kiongozi mwadilifu na anajiheshimu.

No comments:

Post a Comment