Monday, June 25, 2012

Huduma za afya zinaendelea kutolewa



Huduma zinaendelea kutolewa katika baadhi ya hospitali ikiwemo ya Muhimbili na Amana licha ya kutangazwa kwa mgomo wa madaktari Juni 23. Mpaka jana wagonjwa waliendelea kupokelewa na kutibiwa katika hospitali mbalimbali bila matatizo.

Hata hivyo mmja wa madaktari katika hospitali ya Amana ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa mgomo upo na kuongeza kwamba siku za mwisho wa wiki ni madaktari wachache sana wanaofika kazini hivyo si rahisi kutambua kwamba mgomo upo.

No comments:

Post a Comment