Monday, June 25, 2012

Utaratibu wa mabalozi usivurugwe


Msafiri Mtemelwa, Mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi CHADEMA


Msafiri Mtemelwa, Mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi CHADEMA amewataka viongozi wa serikali, watendaji wa vijiji na vitongoji kuwakubali na kutovuruga utaratibu wa mabalozi wa chadema waliowekwa kwa mujibu wa sheria alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana kaitka ofisi za chama hicho za Kinondoni.

Amesema mabalozi wa chadema wamekuwa wakinyanyaswa na baadhi ya viongozi na kuwataka kutofanya hivyo, na kudai kuwa tangu ulipoanza mfumo wa vyama vingi waliiomba serikali kuwaingiza mabalozi katika mfumo wa serikali lakini hawakufanya hivyo.

Msafiri amesema pia chama cha CCM kimekuwa kikitengeneza mfumo wa kulindana katika uongozi na ndio sababu ya chama hicho kuwang’ang’ania mabalozi wa nyumba kumi  kumi kwa kuwa hawakuwa na uhakika wa kutengeneza msingi wao mapema.

CHADEMA inaendelea na uchaguzi wa  mabalozi ulioanza tangu juni mosi mwaka huu na unaendelea mpaka ngazi za juu kwa kuchagua viongozi mbalimbali ndani ya chama.

No comments:

Post a Comment