Machimbo ya Maganza |
Noeli Ganja, Mchimbaji mdogo |
Noeli Ganja akisafisha udongo |
Wachimbaji
wadogo katika machimbo ya Almasi yaliyopo
mji wa Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamesema wanakabiliwa
na wimbi la ushirikina katika utafutaji wa Almasi hatua inayodidimiza maendeleo ya wachimbaji Wilayani humo.
Tatizo hilo linakuja kufuatia kukosekana kwa
vifaa muhimu vya utafiti wa Almasi na kusababisha kuchimba kila mahali bila
kuwa na uhakika wa Almasi.
Licha ya uchawi kutawala shughuli hizo wachimbaji hawa pia wanakabiliwa na uvamizi wa wawekezaji wanaonunua
ardhi kutoka Serikali kuu na wanapoingia katika maeneo yao hutimuliwa bila
kulipwa fidia.
Naye mbunge wa Kishapu Selemeni Masoud Nchambi anaitaka
Wizara ya Nishati na Madini kutenga asilimia 2 ya mapato yatokanayo na Almasi na
kuelekezwa katika maeneo ya uchimbaji ili kutoa motisha kwa wakazi waishio
machimboni.
Kumekuwa
na malalamiko kwa baadhi ya wachimbaji katika maeneo mengi ya uchimbaji hapa
nchini, utafiti uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP umebaini mengi yanayohusu ukosefu wa elimu ya uchimbaji pamoja na migogoro
ya ardhi.
No comments:
Post a Comment