Dr. Steven Ulimboka |
Kiongozi wa jumuiya ya madaktari Tanzania Dr.Stiven ulimboka
amekutwa amejuruhiwa vibaya kutokana na kupigwa na watu wasiojulikana na
baadaye kutelekezwa maeneo ya mabwepande nje kidogo ya jiji la dar es salaam usiku wa kuamkia leo.
Mara baada ya Dr Steven Ulimboka kufikishwa katika chumba
cha dharula katika taasisi ya mifupa
kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili – MOI madaktari wakawazuia waandishi wa
habari kufanya kazi yao.
Sintofahamu hii imekuja baada ya tukio la kushambuliwa kwa
Dr Ulimboka ambaye kwa sasa ni kiongozi wa jumuiya ya madaktari inayoendesha
mgomo wa madaktari hapa nchini.
Kufuatia tukio hilo madaktari na wauguzi walisitisha kutoa
huduma kwa wagonjwa tangu Dr Ulimboka alipofikishwa hospitalini hapo na kuahidi
kuendelea kumlinda usiku kucha.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Naibu
kamishna wa polisi Bw Suleiman Kova amesema, Jeshi lake linaendelea na
uchunguzi wa tukio hilo
No comments:
Post a Comment