Wednesday, June 27, 2012

Mbio Za Mwenge Mkoa wa Dar es Salaam







Jumla ya miradi 28 ya sekta imefunguliwa katika mbio za Mwenge wa uhuru jijini Dar es salaam yenye thamani ya zaidi ya shillingi billion 7 .

Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za mwenge capt. Ernest Mwanossa wakati akikabidhi mwenge kwa kaimu mkuu wa wilaya ya kinondoni Bi: Sofia Mjema mara baada ya kumaliza ziara ya mbio za mwenge katika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

Mwenge huo uliwasili jijini Dar es salaam tarehe 25/06/2012 ukitokea mkoa wa kusini pemba na kuanza ziara ya mbio za mwenge siku hiyo katika wilaya ya temeke, ilala na kukamilisha  ziara hiyo leo katika wilaya ya Kinondoni.

Capt. Mwanossa amesema mwenge huo umebeba ujumbe wa kuhamasisha watu kushiriki katika sensa ya watu na makazi , mchakato wa katiba mpya na mapambano dhidi ya dawa za kulevya na ukimwi.

Nao wakuu wa wilaya za Temeke na  Ilala wamesema Mwenge huo ni kwa ajili  ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja ikiwemo kupambana na rushwa na kuchangia maendeleo katika sekta ya miundombinu na elimu.

No comments:

Post a Comment